Michezo

Shabiki kipofu wa Valencia aliyehudhuria mechi kwa miaka 40, kapewa heshima

on

Club ya Valencia ya Hispania imeamua kumkumbuka kipekee shabiki wake kipofu aliyekuwa anahudhuria kila mechi ya nyumbani ya timu hiyo, shabiki huyo Vicente Aparicio ambaye amekuwa na utamaduni wa kwenda uwanjani kila mechi ya nyumbani kwa kipindi cha miaka 40 Valencia wametambua thamani yake.

Vicente Aparicio alifariki miaka miwili iliyopita akiwa na umri wa miaka 54 na alipoteza uwezo wa kuona 40 iliyopita lakini toka apate ulemavu wa macho alikuwa haendi uwanjani anafulia mechi za Valencia kwenye TV ndipo 1994 alipoamua kukata tiketi ya msimu na kuwa anahudhuria kila mechi ya nyumbani ya Valnecia.

Mtoto wa Vicente Aparicio akiwa katika sanamu ya baba yake katika uwanja wa Mestalla.

Kwa heshima hiyo Valencia wameamua kumjengea sanamu Vicente Aparicio ndani ya uwanja wa nyumbani wa Valencia Mestalla siti 164 ambayo alikuwa akipenda kukaa  wakati wote wa uhai wake, licha ya kukosa uwezo wa kuona lakini hakukauka Mestalla kuangalia game.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments