Top Stories

Ugonjwa ulivyombadilisha na kuwa kama ‘Nyani’, hautibiki (+Video)

on

Anaitwa Lalit Patidar ni kijana mwenye umri wa miaka 13 ni raia wa India. Latit alizaliwa akiwa na ugonjwa wa Hypertrichosis ambapo dalili zake hutajwa kuota nywele sehemu ambazo sio za kawaida mwilini mfano usoni, mikononi na sehemu nyingine za mwili.

Ugonjwa huu umemfanya Lalit kuonewa sana akiwa shuleni ambapo wanafunzi wenzake humrushia mawe na kumuita nyani, hali hii imemfanya Lalit kufikiria kuja kufanya upasuaji siku moja ili kuondoa nywele zote usoni ili marafiki zake wapate nafasi ya kucheza nae bila uoga.

Latit ana ndoto ya kuja kuwa polisi ili awakamate waarifu na kuwafunga anaamini kupitia kazi hiyo atapata fedha nyingi za kuwasaidia wazazi wake.

Bonyeza PLAY hapa chini kutazama ugonjwa huo wa ‘ Hypertrichosis’ ulivyomuathiri Latit

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA JAMAA ALIAGIZA HELIKOPTA IMCHUKUE MPENZI WAKE, BAADA YA SAA 5 KWENYE FOLENI?

Soma na hizi

Tupia Comments