Wananchi wa Bumbwini Makoba Mkoa wa Kaskazini “B” Unguja wameanza kupatiwa huduma za Dawa kwa magonjwa yasio ambukiza yakiwemo Kisukari na Presha kwa Vikundi ,ambapo kwa maara ya kwanza utoaji wa Huduma za Dawa kwa Vikundi kuanza kutumika Bumbwini Mkoa wa kaskazini.
Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe Nassor Ahmed Mazrui, amesema wataendelea kushirikiana na shirika la Pharm Access ili kuona wanaendelea kuwapatia huduma wananchi za afya zinaimarika nchini na kuendelea kutolewa kwa wakati.
Alisema, magonjwa yasiyoambukiza kwa sasa ni tishio Zanzibar ambao kwa sasa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameweka mipango madhubuti ili kuona wanapambana na maradhi hayo..
Pharm Access kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar kwa pamoja wanakusudia kuimaliza changamoto zinazojitokeza pindi wagonjwa wa Kisukari na Presha wanapokwenda kufuata Dawa zao magonjwa hayo kutokana na Foleni zinazojitokeza
Akitoa ushuhuda wa upatikanaji wa huduma zinazotolewa, Jafari Iyombwe Haji, alishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Wizara ya ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Pharm Access kwa kuwapelekea huduma katika kijiji chao kwani imewarahisishia upatikanaji wa huduma ambapo awali walikuwa wakipata usumbufu.