Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Membe amefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusubiri hukumu yake dhidi ya Cyprian Musiba.
Hukumu hiyo ni ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018 ambapo kesi hiyo iliyoitwa kwa mara ya kwanza Februari 26, 2019,
Katika kesi hiyo Membe amemshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo anawadai Sh. Bilioni 10 kwa kumchafua.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa mbele ya Jaji Joacquine De Melo.
Musiba katika kesi hiyo anashtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.