Habari za Mastaa

Mauzo ya R. Kelly yaongezeka

on

Mauzo ya muziki wa Msanii Robert Kelly (R. Kelly) yameongezaka kwa zaidi ya asilimia 500 tangu staa huyo wa R&B alipokutwa na hatia katika kesi ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake.

Kwa mujibu wa jarida la Rolling Stone, mauzo ya kazi za R. Kelly mwenye umri wa miaka 54 yamepanda kwa asilimia 517.

Msanii huyo mzaliwa wa Chicago, alikutwa na hatia Septemba 24, mwaka huu, na kama si miaka miaka 10 gerezani, basi atahukumiwa kifungo cha maisha.

Mei 4, mwakani, ndiyo siku ya hukumu yake na ndipo atakapoangukiwa na moja kati ya adhabu hizo.

MWAMBA WA MIUJIZA, MAJINI, UNAMEZA WATU KICHAWI, MELI ILIZAMA “WANAFUNZI WALIMEZWA, WATU WANAKUFA”

Soma na hizi

Tupia Comments