Club ya Aston Villa leo imefanikiwa kurudi kucheza Ligi Kuu England kwa msimu wa 2019/2020 baada ya kufanikiwa kupata ushindi katika game ya Play Off iliyochezwa katika uwanja wa Wembley dhidi ya Derby County club ambayo inafundishwa na Frank Lampard.
Game ya leo ilikuwa inazikutanisha timu ambazo zinafundishwa na makocha ambao wote wamewahi kucheza kwa pamoja katika kikosi cha timu ya taifa ya England na Club ya Chelsea, Aston Villa walikuwa na John Terry wakati Derby County walikuwa na Frank Lampard.
Hata hivyo kikosi cha Aston Villa ndio kilifanikiwa kupanda Ligi Kuu kwa kuifunga Derby County kwa magoli 2-1, magoli ya Aton Villa yakifungwa na El Ghazi dakika ya 44 na McGinn dakika ya 59, wakati goli la kufutia machozi la Derby County likifungwa na Marriot dakika ya 81.
Baada ya ushindi huo Aston Villa wanapokea kiasi cha pound milioni 170 ikimo pound milioni 95 za kupanda kucheza Ligi Kuu ya England, kiasi cha pesa kinaweza kupanda zaidi kama Aston Villa watafanikiwa kuendelea kuwa juu ikiwemo kusalia katika EPL kwa msimu ujao.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega