Baada ya kuitumikia club ya FC Bayern Munich ya Ujerumani kwa miaka nane beki wa timu ya taifa ya Ufaransa Jerome Boateng imeripotiwa kuwa kaambiwa atafute timu, Boateng alikuwa miongoni wa mabeki tegemeo katika kikosi cha FC Bayern lakini inaonekana kuna dalili zote kuwa msimu wa 2019/2020 hatoendelea kuichezea timu hiyo.
Taarifa hizo zimeripotiwa kutolewa na Rais wa FC Bayern Uli Hoeness ni kuwa staa huyo aanze kutafuta timu mpya ya kuichezea, Boateng msimu huu amekumbwa na wakati mgumu wa kupata majeraha yaliopelekea kupata nafasi ndogo ya kuanza katika michezo nusu ya Bundesliga, Mr Uli Hoeness (67) alizungumza maneno hayo wakati wa sherehe za Ubingwa Jumapili iliyopita.
“Ningemshauri ahame club kwa sababu nahisi anahitaji changamoto mpya, mimi kama rafiki ningemshauri atafute club mpya mwenyewe milango haijafungwa ila ana mkataba vile vile”>>>>>Uli Hoeness
Jerome Boateng mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa, msimu uliopita alikuwa anahusishwa kwa karibu kutaka kujiunga na club za Man United na Paris Saint Germain, Boateng alijiunga na club ya FC Bayern 2011 akitokea Man City ya England aliyokuwa kaichezea kwa takribani msimu mmoja tu.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega