Kiungo wa zamani wa club ya FC Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Hispania Xavi Hernandes ameweka wazi kuwa kwa sasa anaonda ndio wakati muafaka kwake, kuamua kutundika daruga na kuendelea na maisha mengine nje ya kucheza soka kama tulivyomzoea.
Xavi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 39 akiichezea timu ya Al Saad SC ya Qatar, ameweka wazi kuwa huu ndio msimu wake wa mwisho katika soka akiwa kama mchezaji, baada ya hapo ataendelea na maisha mengine ila kwa soka amemaliza na anaona ni wakati sahihi kwake kupumzika.
Kiungo huyo aliondoka FC Barcelona na kwenda Qatar 2015 baada ya kudumu na FC Barcelona tokea timu za vijana 1991, Barcelona B 1997-1999, timu ya wakubwa kuanzia 1998 hadi 2015, Xavi anastaafu akiwa kadumu na Al Saad SC kwa miaka minne, hadi anaondoka FC Barcelona 2015 alikuwa ametwaa jumla ya mataji 24.
Mataji aliyoshinda ni 8x La Liga, 3x Copa del Rey, 4x UEFA Champions League, 2x FIFA Club World Cup, 6x Spanish Super Cup, 2x UEFA Super Cup, six-time Copa Catalunya na 1x Catalunya Super Cup, Xavi ndio anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi Barcelona akiwa amecheza jumla ya game 767 na kafunga magoli 85.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania