Leo January 18, 2019 tunayo video iliyomnasa msanii wa maigizo Lucas Mhavile maarufu kama Joti akiwa katika Jengo la Mahakama ya Watoto iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuti jijini Dar es Salaam.
Joti anadaiwa kufika mahakamani hapo majira ya saa 1 asubuhi na kuelekea katika jengo hilo la Mahakama ya Watoto, ambapo inadaiwa kilichomfikisha mahakamani hapo ni kutofautiana na mzazi mwenzie juu ya kumlea mtoto(Mpango wa Kando).
Joti na mzazi mwenzie walionekana wakiingia katika viunga vya mahakma hiyo majira ya saa 1 asubuhi na kuelekea katika jengo la Mahakama ya Watoto ambapo waliondoka maeneo hayo majira ya alasiri.
Hata hivyo, Joti hakuweka wazi kisa na mkasa kilichomfikisha yeye na mzazi mwenzie mahakamani hapo badala yake aliwakimbia Waandishi wa Habari, licha ya kuwa taarifa za awali zinadai kwamba Joti amemshitaki mzazi mwenzie kisa kupokonywa mtoto.