Golikipa wa timu ya taifa ya Senegal Khadim N’diaye aliyekuwa sehemu ya kikosi cha club ya Horoya AC ya Guinea kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali ya club Bingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca sasa ni wazi atakosa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Misri baada ya kupata jeraha la kuvunjika mara mbili mguuni.
Khadim N’diaye katika mchezo huo uliomalizika kwa timu yake kupoteza kwa magoli 5-0 (agg 5-0), akijaribu kuokoa mpira ambao baadae ulifungwa na kuwa goli la tano, aligongana na mchezaji mwenzake Boubacar Samassekou na kuvunjika mguu wake wa kulia mara mbili.
Sasa ni wazi kutokana na jeraha lake hilo alilolipata ambalo Khadim litamuweka nje kwa miezi sita ni wazi atakosa michuano ya AFCON 2019, tukio la N’daye limeripotiwa kuwagusa wengi kiasi cha shirikisho la soka Morocco kudaiwa kuwa limeahidi kugharamia matibabu ya mchezaji huyo.
Club yake ya Horoya AC imeamua kumpa mkataba mpya wa miaka mitatu na kumpa ofa ya kugharamia masomo yake ya ukocha akistaafu soka, N’diaye kwa sasa ana umri wa maika 34 na kutokana na jeraha lake alilolipata wengi wanaamini inaweza ikawa ndio mwisho wake katika kazi yake ya soka.
Kocha wa Serengeti Boys Oscar Mirambo kaongea baada ya kipigo 5-4 vs Nigeria