Michezo

Raiola akutana na Mkurugenzi wa PSG katika chumba cha hoteli kisa De Ligt

on

Wakala maarufu wa wachezaji soka mbalimbali duniani Mino Raiola imeripotiwa kuwa yupo mbioni kukamilisha dili la kuumuza beki wa Ajax na timu ya taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt  kwenda club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Raiola imeriporitiwa kuwa kwa usiri mkubwa amekutana na mkurugenzi wa Paris Saint Germain katika chumba cha hoteli kwa ajili ya kujadili uhamisho wa Matthijs de Ligt kwenda PSG pamoja kuwa FC Barcelona nao wanaripotiwa kuwa na nia na beki huyo bora akiwa na umri wa miaka 19.

Ajax inaripotiwa kuwa wanahitaji pound milioni 66.5 kwa ajili ya kutoa baraka kwa nahodha wao Matthijs de Ligt kujiunga na PSG, Matthijs de Ligt ambaye ameichezwa Ajax zaidi ya michezo 100 hadi sasa mkataba wake na Ajax unamalizika 2021 na msimu huu amekuwa gumzo kwa kuisaidia timu hiyo kufika nusu fainali ya UEFA Champions League.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments