Mwanadada Vera Sidika kutokea Kenya amerudi tena kwenye headlines Afrika Mashariki baada ya kuonekana kuwa karibu na mwimbaji wa muziki kutokea nchini Jimmy Chansa na wengi kupiga mstari kuwa wawili hao ni wapenzi.
Vera Sidika ambaye siku kadhaa alizua gumzo baada ya kuonekana kuwa amebadilisha rangi ya ngozi yake kutoka kuwa mweupe na kuwa mweusi amezidi kuweka kitendawili kwa mashabiki zake kutokana na picha pamoja na videos ambazo amezipost kupitia insta story yake zikimuonyesha akiwa na Jimmy Chansa.
Mwimbaji Jimmy Chansa ambaye alitamba na ngoma ya ‘We Mchoyo’ ameonekana kuwa karibu na mwanadada huyo kutokea Kenya na wengi kuhoji inawezekana ikawa ni kolabo kati yao au ni kiki na pengine ni penzi jipya kati ya Tanzania na Kenya.
UMEPITWA NA HII VIDEO YA UWOYYA AMWAGA PESA KWA WAANDISHI, AVURUGA MKUTANO? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA