Fahamu kuwa Rapper Tory Lanez hakupendezwa na kitendo cha muongozaji wake kumuondoa video vixen aliyekuwa na asili ya Kiafrika na kumuweka mwingine mwenye asili ya kizungu wakati waki-shoot, Tory aliamua kusimamisha maandalizi ya video yake mpya baada ya muongozaji huyo kuonyesha kitendo cha ubaguzi wa rangi.
Rapper huyo aliamua kutupia video fupi kwenye ukurasa wake wa instagram ikimuonyesha muongozaji huyo kuchukua maamuzi ya kufanya mabadiliko ya video vixen na ndipo Tory aliposhindwa kuvumilia kitendo hicho na kusimamisha shughuli hiyo kwa muda.
Tory Lanez aliamua kuandika caption yenye ujumbe mrefu kuhusu ubaguzi wa rangi unaofanyika kwenye industry ya muziki nchini Marekani na kuwataka wasanii waungane na kupiga vita vitendo hivyo vinavyofanywa hasa na waongozaji wa muziki (directors).
“Hili ni tatizo linaloendelea kwenye jamii zetu na inatakiwa kuachwa, mimi kama mwanaume mwenye asili ya Kiafrika mara nyingine huwa nafanya utani kuhusu jamii za watu weusi kama ambavyo wengi tunafanya lakini ambacho siwezi kufanya ni kuruhusu hawa waongozaji kuwashusha thamani wanawake wetu weusi”
“Mara nyingi sana nimeona waongozaji wakibadilisha wanawake weusi na kuwaweka weupe au kuwaweka wanawake wenye nywele zilizonyooka, ni jukumu letu kama wasanii kusimama na kutoruhusu kitu kama hiki kufanyika, ni muda sasa umefika wa kujivunia wanawake wetu wenye asili ya Kiafrika” >>> aliandika Tory Lanez
AUDIO: ULIPITWA NA HII YA MUIGIZAJI WEMA SEPETU KUPELEKWA GEREZANI SIKU 7? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUFAHAMU