Club ya Real Madrid ya Hispania kwa pamoja ziliwapoteza wote wawili Cristiano Ronaldo aliyemaua kujiunga na Juventus na kocha wao Zinedine Zidane alyeamua kustaafu baada ya kutwaa mataji matatu mfululizo wa UEFA Champions League, hivyo alijiuzulu kulinda heshima yake baada ya kupata mafanikio ya kipekee.
Baada ya kuwakosa wawili hao ambao walikuwa muhimu katika club yao, wengi wamekuwa wakijiuliza Real Madrid inawakumbuka wakali hao? Ronaldo inadaiwa kuwa aliondoka baada ya kutoelewana na Rais wa Club hiyo Fiorentino Perez wakati Zidane aliondoka kulinda heshima yake akiona kuwa hakuna alichobakiza.
Real Madrid alianza kuondoka Zidane na wiki kadhaa baadae Ronaldo nae akaondoka na kwenda kujiunga na Juventus kwa pound milioni 105, hata hivyo vyanzo vya ndani ya club vinaeleza kuwa Real Madrid inakumbuka zaidi na kumuona muhimu Zidane zaidi ya Ronaldo alivyokuwa ameamua kuondoka.
Hata hivyo Real Madrid bado inaendelea kupambania kuwa katika kiwango chake ikiwa chini ya Santiago Solari ambaye pia ametajwa kuwa hawaoni kama ana sifa za kuendelea kuwa kocha mkuu wa Real Madrid kwa msimu ujao zaidi, kwa sasa Real Madrid ipo nafasi ya 3 katika LaLiga, point 45, wameshinda michezo 14, sare 3 na wamepoteza game 7.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba