Uongozi wa English Football League imeamua kufikia maamuzi ya kuiadhibu club ya Leeds United kwa kosa la kupeleleza mazoezi ya Derby County, inaelezwa kuwa watu wa benchi la ufundi la Leeds walionekana nje ya uwanja wa mazoezi wa Derby County ikielezwa kuwa wameenda kuipeleleza club hiyo.
Uongozi wa EFL kutokana na kubaini Leeds United kufanya hivyo yaani kupeleleza mazoezi ya Derby County January 10, wamefikia maamuzi ya kuwapiga faini ya pound 200000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 600 kwa kosa hilo ambalo kwa kawaida ni kinyume cha sheria za soka kupeleleza mazoezi ya wapinzani wako.
Imeripotiwa kuwa kocha wa Leeds United Marcelo Bielsa amekuwa na utamaduni wa kutuma watu kuwapeleleza wapinzani wake siku chache kabla ya kucheza nao, hivyo alituma wafanya hivyo siku chache kabla ya kucheza na Derby County January katika mchezo wao wa Championship ikiwa ni mbio za kuwania kupanda kucheza Ligi Kuu England.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba