Kwa mara ya kwanza Tanzania inapata ushiriki wa nafasi nne kwa vilabu vyake kucheza michuano ya kimataifa inayoandaliwa na shirikisho la soka Afrika CAF, Tanzania sasa katitka msimu wa 2019/2020 itawakilishwa na Simba SC na Yanga SC katika michuano ya CAF Champions League wakati michuano ya CAF Confederation Cup itawakilishwa na Azam FC na KMC.
Hii wadau na wapenzi wa soka wanaitafsiri kama nafasi adimu na heshima kubwa kwa taifa la Tanzania kupata ushiriki wa timu nne kwa mara moja, afisa habari wa Simba SC Haji Manara kutokana na hilo ametangaza wazi kuwa ameanza kuzisapoti kwa kujitolea timu zote nne ikiwemo Yanga SC watu waende uwanjani kwa sababu hilo ni suala la nchi.
“Tunaamini baada ya mchezo wa Jumamosi moja kati ya kazi ambazo bwana Clifford na TFF mniruhusu kwa kushirikiana na wenzangu hawa tuna mechi tatu za nyumbani za club za Tanzania (Simba, Azam na KMC) na moja ya ugenini(Yanga) tuzunguuke katika radio zote tufanye press conference kuhimiza watu waziunge mkono timu zetu katika michuano ya kimataifa”>>>Manara
VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS