Habari za Mastaa

Rapper Jimmy Wopo afariki kwa kupigwa risasi

on

Baada ya taarifa za Rapper chipukizi Xxxtentacion kufariki dunia kwa kupigwa risasi June 18,2018 hii ni taarifa nyingine ya msiba kutoka kwa Rapper Jimmy Wopo ambaye amefariki muda mchache baada ya kupigwa risasi June 18,2018.

Jimmy Wopo amepigwa risasi na kufariki na watu wasiojulikana akiwa kwenye mji wa Piitsburgh na imeripotiwa  kuwa katika tukio hilo kuna baadhi ya watu wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali na hali zao kwa sasa zinaendelea vizuri.

Rapper huyo enzi za uhai wake ametambulika na ngoma zake kibao zikiwemo Elm Street, Prime Time, Lost, Ayo na nyingine nyingi na amefariki akiwa na umri wa miaka 21.

Jibu la Vanessa kwa shabiki aliyemuambia hajui kuimba Live

Soma na hizi

Tupia Comments