Habari za Mastaa

Idris Sultan kahojiwa Kenya kuhusu Wema Sepetu na ile video iliyosambaa.

on

Kumekua na stori zinaendelea mitandaoni na hasa ni baada ya Mwigizaji Wema Sepetu aliyekaa sana kwenye vichwa vya habari hivi karibuni kwa kuwa mapenzini na mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014 Mtanzania Idris Sultan ambapo stori hizo ni baada ya Wema kuonekana akimbusu mwanaume.

Baada ya hayo, Idris amehojiwa na mtangazaji Larry Madowo wa The TREND NTV Kenya na kusema yafuatayo >>>Ile video ilipopostiwa na kila mtu kuanza kuiongelea ndio na watu kuanza kuja kwangu kuniita Bwege sababu siwezi kumuongoza Mwanamke wangu anachukuliwa na siwezi sifanya chochote, niliongea na Wema baada ya hii video lakini hatukuongea vizuri akanipa attitude, kilichonifanya nijisikie vibaya sio lile busu pekee, ni sababu kwanini video ipo mitandaoni

Siwezi kusema tumeachana na Wema lakini ukweli ni kwamba hatuna maelewano, sio kwamba najaribu kusema Wema ni mtu mbaya… ni mtu poa na ile video inawezekana hata hakujua inapostiwa kwenye mitandao, tatizo lilikua ni pale nilipompigia ingetakiwa tufikie kwenye maelewano na sio attitude‘ – Idris

https://www.youtube.com/watch?v=acF8E4SyudI

JIONEE PARTY YA INSTAGRAM MWANZA.. WEMA SEPETU NA WATU WAKE

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments