Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema ushirikiano wa nchi za Tanzania, Burundi Na DRC hasa kitengo cha ulinzi na usalama utamaliza matukio ya ugaidi na utekaji na kwamba hatua hii ni endelevu kwa nchi zote 3 kumaliza kabisa matukio ya kiuhalifu.
IGP Sirro amesema hayo katika kikao kazi cha usalama kwa Nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, kilichofanyika Mkoani Kigoma kikiwa na lengo la kuimarisha usalama mipakani na kukabiliana na wahalifu kutoka Nchi hizo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Burundi CPP Melchiade Ruceke ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa kinara wa kuchochea amani kwa Nchi hiyo na kubainisha kuwa watadumisha amani na kuibua wahalifu ili kudumisha.
MAAMUZI YA MAHAKAMA KWA KIGOGO ALIYEMBAKA MTOTO WAKE