Leo February 5,2018 story ambayo imechukua headlines katika mitandao ya kijamii ni hii ya msanii kutoka Bongo flevani Gigy Money ambaye caption katika instagram page yake imezua maswali kwa mashabiki na kuleta utata.
Gigy Money kwa sasa ni mjamzito na anategemea kupata mtoto hivi karibuni na amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji wa Choice Fm maarufu kama Mo J kwa kipindi kirefu sasa.
Kupitia instagram page yake Gigy Money ameandika caption yenye maneno mazito inayosemekana kuwa anaweza akawa ameumizwa katika mapenzi ikiwa bado ni mjamzito na ndio maana akaamua kuweka wazi kupitia instagram account yake.
“Kiukweli leo nina stress sana na ndio mana nimeona bora niseme kwani nachokiamini mm sio peke angu ninayo yapitia haya kuna muda unaweza ukakufuru mungu kwa maneno ambayo kesho na kesho kutwa huwezi kuyarudisha kinywani”
“Katika makosa ambayo najua nimeyafanya nikupenda lakini kupenda sio dhambi nimepitia mengi sana kwenye Mapenzi kiasi cha kufikia kupungua kimwili hakuna kitu kibaya na kigumu kama kumuaminisha mtu unampenda unaweka nguvu na jitihada zako katika mapenzi”
“Kuna muda unawaza sijui niachie ngazi kwani unaempenda yawezekana anampenda mtu mwingine na anaekupenda humpendi hata kidogo ??inafurahisha nakustaajabisha lakini naweza kukiri kwamba jamani nilipenda nimepitia vingi sana kwa watu walio karibu na mimi wanaweza wakawa wanajua#was“
“Baadhi ya mateso na utumwa wa mapenzi niliowahi kupitia na bado najiuliza kwa nini wanaume ni wagumu kuonesha hisia zao za ukweli inashangaza mwanaume anaweza kuishi na wewe pika pakua lakini anaempenda yuko mbali na upeo wa macho yake hicho kitu naamini”
“Wanawake wengi hawakiwezi ikiwa mimi ni mmoja wao kama sikutaki nitakwambia in good way bila hata kugombana lakini mwanaume hawezi kuwa muwazi na hii labda anapata kitu kidogo kwako yawezekana pesa, mavazi au umaarufu yote yanawezekana”
“Kiukweli natamani ningekuwa gigy yule ambaye naweza kuwa na maamuzi yangu binafsi lakini nashindwa naumia mapenzi ni kitu ovyooooo na mara nyingi huwaga tunawapenda watu wenye uwezo wa kawaida tukiamini mapenzi sio pesa ila wanaume wabongo wajeuri”
“Unabeba mimba dharau atakufanyia mwanamke wake wa nje atakuonesha kiukweli inauma ndio lakini naamini ni hatua za maisha na ukuaji naamini nimedondoka hatua moja lakini naweza kuinuka hatua 8”
“Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na single mother’s sio wote baba wa watoto wamefariki wengi wetu huwaga tuna wakimbiza watoto wetu mbali na maisha na mateso tuliyowahi kuyapitia kwa baba zao hakuna mtu anayeweza kunielewa”
“Mkiona mtu Ana type hivi ujue yanazidi hakuna kitu kibaya kama mtu akupendee kitu inauma sana #nachukiamwanaumeanaepigawanawakewajawazito #nachukiawanaumewanyanyasaji#sikilamwanaumeanayosifayakuiitwamume GOOD NIGHT”
Tunda “Diamond nipo nae karibu, nionane na Zari ili niongee naye nini?”