Mix

PICHA 9: Rais Magufuli alivyokutana na mabalozi na katibu wa SADC Ikulu walichokizungumza……

on

May 19 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na mabalozi mbalimbali pamoja na katibu mtendaji wa SADC Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo.

Baadhi ya mambo waliyozungumza ni pamoja na mpango wa kuanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2016 wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

Kiwanda hicho kitatumia rasilimali ya gesi asilia  na miamba ya  matumbawe ‘coral reef’ iliyopo wilayani Kilwa, kitajengwa kwa ubia kati ya Tanzania na nchi za Dernmark, Ujerumani na Pakstani na kitakuwa na uwezo wa kuzalishatani 3800za mbolea kwa siku. 

2

Rais Magufuli na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Egon Kochanke

5

Rais Magufuli na Balozi wa Uturuki hapa nchini Yasemin Aralp .

6

Rais Magufuli na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd .

8

Rais Magufuli na Katibu Mtendaji wa SADC Dk. Stergomena Tax

3

Balozi wa Ujerumani hapa nchini Egon Kochanke akimkabidhi Kitabu kinachohusu masuala mbalimbali ya Ujerumani Rais Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo 

9

Rais Magufuli, Katibu Mtendaji wa SADC , Stergomena Tax pamoja na Maafisa wengine kutoka Ikulu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

4 7 10

ULIKOSA KILICHOMCHEKESHA RAIS MAGUFULI JAPOKUWA ALIKUWA KAVAA SURA YA KAZI IKULU? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments