Mix

Ripoti ya Mauaji ya kuchinjwa watu 3 ndani ya nyumba ya Ibada (Msikiti) Mwanza.

on

Taarifa iliyonifikia kutokea Mwanza ni hii ya kusikitisha ya watu watatu kuuawa kwa kuchinjwa wakiwa katika nyumba ya ibada usiku May 18, 2016,  Msikiti wa RAHMAN eneo la Ibanda relini mtaa wa Utemini Mkolani Mwanza.

Ripoti kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza Ahmad Msangi amesema……>>>Watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso, wakiwa na Mapanga, Shoka na Bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia msikitini wakati waumini wakiwa wanaswali wakazima taa wakisema Kwanini mnaswali wakati wenzenu wanashikiliwa na Polisi?’

Image00001 - Copy

Msikiti wa RAHMAN ambapo tukio limetokea

Waliouawa 1.Feruz Ismail Elias (27) Imamu wa Msikiti, 2.Mbwana Rajabu (40), 3.Khamis Mponda (28) pamoja na Ismail Abeid (13) aliyejeruhiwa mwanafunzi wa shule ya Jabar Hila Nyasaka, anapata matibabu kwenye Hospital ya Nyamagana ;- Kamanda Ahmad Msangi

Image00003 - Copy

Watalaamu wamefika kufanya uchunguzi kwenye hilo tukio

Waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wahalifu wakikimbia na kurusha chupa mbili za Konyagi ndani ya Msikiti zikiwa na Petroli pamoja na tambi moto, chupa moja ililipuka ila haikuleta madhara makubwa’;Kamanda Ahmed Msangi

Image00004 - Copy

ULIIKOSA HII YA MAZISHI YA WATU WATANO KATI YA SABA WALIOKATWA MAPANGA SENGEREMA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments