Michezo

Inonga na Ahmed Ally waupiga mwingi mwezi April Simba SC

on

Beki wa Simba SC Henock Inonga Baka raia wa Congo DR amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi April wa mashabiki wa Simba SC kutokana na kuonesha kiwango bora.

 

Inonga amepewa tuzo ya Emirate Alluminium ACP pamoja na kitita cha Tsh milioni 2 kama zawadi kutoka na kiwango bora alichoonesha ndani ya mwezi April.

Pamoja na kuwa na kiwango bora kwa muda mrefu Inonga katika derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga iliyochezwa April 30 2022 na kumalizika kwa sare 0-0, Inonga  alionesha kiwango bora kwa kumdhibiti Fiston Mayele kutoonesha makali yake.

Hata hivyo Emirate Aluminum ACP ambao ndio wadhamini wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Simba SC, wametambua mchangoa wa meneja wa habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally wa hamasa kwa mashabiki na kumpa zawadi ya Tsh milioni 2.

Soma na hizi

Tupia Comments