Hii ndio Ripoti mpya kuhusu idadi ya watumiaji wa #INSTAGRAM Duniani kwa sasa..
Share
3 Min Read
SHARE
Katika Mitandao ya Kijamii iliyobeba umaarufu mkubwa Duniani, Facebookilianzishwa February 2004, Twitterilianzishwa March 2006 hiyo ilikuwa miaka miwili mbele ya Facebook… Instagramimechukua umaarufu mkubwa sana sasahivi kwa sababu watu wengi wanapendelea kushare pichaz na watu wao, Insta ilianzishwa mwaka 2010 na kuanza kuchukua headlines mdogomdogo !!
Ripoti mpya imetoka na imethibitishwa na Wamiliki wa Instagram wenyewe, taarifa ikufikie kwamba Instagramimefikia hatua ya kuwa na watumiaji MILIONI 400 mpaka kufikia September 22 2015, hiyo ni ndani ya miaka mitano tangu Mtandao huo umeanzishwa.
Kwa Takwimu hizo ni kwamba mpaka sasahivi, Instagram umekuwa Mtandao ambao umekua kwa kasi zaidi ndani ya kipindi cha miaka mitatu ambapo watumiaji wake wanakaribia kufikia hesabu ya watumiaji wa Twitter ambao wanakadiriwa kuwa MILIONI 500 Duniani kote.
Instagram ni kama ilipata nguvu zaidi na umaarufu kuanzia mwaka 2012 ambapo wamiliki wa Facebook waliinunua Instagram kwa Dola Bilioni Moja ambazo kwa TZ inagusa karibia Trilioni 2.2 kwa hesabu ya sasahivi!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>>TwitterInstaFB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE