Moja kati ya vitu vilivyowahi kudaiwa vinaitawanya Man United ni ugomvi au vita ya chini kwa chini kati ya kocha wa zamani wa Man United raia wa kireno Jose Mourinho dhidi ya kiungo wake raia wa Ufaransa mwenye asili ya Guinea Paul Pogba kutokuwa katika maelewano mazuri.
Mwanzoni vita ya Jose Mourinho dhidi ya Pogba ilianza baada ya kudaiwa kumchezesha mchezaji huyo katika nafasi ambayo asioipenda lakini ikafikia hatua watu wakaanza kudai kuwa kati ya Jose Mourinho na Pogba ni lazima mmoja aondoke katika timu, ndio miezi michache baadae ikadaiwa wachezaji hawamkubali Mourinho na timu ikamfuta kazi na kurithiwa kwa muda na Ole Gunnar Solskjaer.
Baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho, kiungo Paul Pogba amekuwa na wakati mzuri sana ndani ya club ya Man United, kiasi cha kudiriki kutajwa kuwa amekuwa na wakati mzuri zaidi katika maisha yake yote ya soka Old Trafford, Pogba leo alikuwa sehemu ya kikosi cha Man United kilichocheza dhidi ya Fulham ugenini na kupata ushindi wa magoli 3-0.
Magoli ya Man United yakitiwa wavunia na Paul Pogba dakika ya 14 na 65 kwa mkwaju wa penati baada ya Anthony Martial kufunga goli la pili dakika ya 23, na kuifanya Man United kurudi TOP 4 huku ikiiombea Chelsea matokeo mabaya katika mchezo dhidi ya Man City ikiwa imewazidi point moja na mchezo mmoja, Pogba sasa ndani ya game 10 chini ya Solskjaer anafunga magoli 8 na assist 5 licha ya kuwa Mourinho kudaiwa kumuona mchezaji huyo kama kirusi aliyekuwa anaitawanya timu.
“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji