Wanasema mapenzi ni kikohozi……….. kukificha ameshindwa Juma Jux ambapo mwimbaji huyu wa Bongofleva ameielezea kumbukumbu yake kubwa kwenye siku yake ya kuzaliwa na kumkumbu mtu aliekua muhimu sana kwenye maisha yake.
Moja ya sababu aliyodai Jux ni kuwa mapenzini na mwanamke ambaye alikuwa faraja kwenye maisha yake ambapo kila ilipofika siku ya kukumbuka kuzaliwa kwake aliridhika na text zake au kuongea naye hata kwa simu na kumtosha.
“Nakumbuka mara ya mwisho kufanya party ya Birthday yangu ilikuwa 2013, Miaka minne iliyopita. Sikuwahi kufanya party yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yoyote kwenye maisha yangu. Miaka yote iliyofata nilikuwa na yeye mpaka sasa atuko tena karibu kama mwanzo, Tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu ???.”
“Uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, Kuongea na yeye au txt yake tu ilitosha kukamilisha siku yangu. Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo ???. Nitafarijika sana kama nitamuona hiyo siku. This time nataka kuparty na watu wangu nani anataka kuparty na mimi katika siku ya birthday yangu ?” – Juma Jux.
.
NIYONZIMA KAFUNGUKA: Ni kuhusu uhusiano wake na Jini Kabula, mkewe je?
VideoFUPI iliyosambaa !! Ni harusi ya Diamond na Zari?
HAUTAKI KUPITWA??? Kuna hii APP MPYA YA MILLARD AYO kwa wewe wa ANDROID unaweza kubonyeza hapa moja kwa moja kwenda kui-download mtu wangu, HABARI ZOTE KIGANJANI MWAKO >>> APP MPYA BONYEZA HAPA