Inawezekana ukawa na maswali kwamba kwanini muziki wa Hip Hop bado haujatusua kimataifa sasa Emmanuel Simwinga aka Izzo Bizness amefunguka na kuelezea sababu zinazopelekea kwa kukwama.
‘Muziki wa Hip Hop sio kama Haupenyi kimataifa ila kuna vitu ambavyo vinakwamisha kama uongozi mbaya, mtaji mdogo kwahiyo kuna vitu vingi lakini sio kwamba muziki wetu haupenyi au hauwezi kufika ukapendwa hapana labda sasa hivi tukamzungumzia Joh Makini anafanya rapper anafanya Hip Hop na tunaona anapata rotation nzuri tu TV kubwa na wimbo wake wa Nusu Nusu hiyo inaonesha kabisa ni njia kwa wasanii wengine ambao wanafanya muziki kama wa Joh Makini’ – Izzo Bizness
‘Na yeye pia amewekeza kwenye biashara yake ile kwa hiyo point ya msingi ni connection kuwa na mtaji wa kutosha wa kuendesha biashara yako wa kupiga ngoma kali mbona tuko huku tunawajua wakina Ice Prince, Sarkodi ni ma rapper wa Africa wanao rapper kwa hiyo tufika tu cha msingi ndio kama hayo mambo niliyoyataja’ – Izzo Bizness
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie