Jana jioni February 26 2019 tasnia ya habari na burudani ilimpoteza mmoja kati ya watu muhimu ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba, marehemu Ruge Mutahaba amefariki akiwa anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
Club ya Simba SC ambayo ndio club aliyokuwa anaishabikia marehemu Ruge Mutahaba, imeeleza kupokea taarifa za kifo cha Ruge Mutahaba kwa masikitiko makubwa, sambamba na kutuma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.
Video:Dakika 2 za Joseph Kusaga kufuatia kifo cha Ruge Mutahaba