Habari za Mastaa

BREAKING: Sam wa Ukweli afariki Dunia

on

Msanii wa Bongo Fleva, Salum Mohamed maarufu ‘Sam wa Ukweli’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo June 7, 2018  katika hospitali ya Palestina, Sinza baada ya kuugua.

Taarifa kutoka kwa Mtayarishaji wa nyimbo zake aliyefahamika kwa jina la Steve amesema Sam alianza kulalamika maumivu ya tumbo tangu Jumanne hadi alipozidiwa Jumatano usiku.

Sam alionekana kusumbuliwa na tumbo hilo kwa muda mrefu maana lilipoanza kumuuma alidai huwa anakunywa vitu vya moto na anapona, hivyo Steve na wenzake walifanya harakati za kumtafutia supu.

Bonyeza PLAY kumsikiliza STEVE aliyekuwa na marehemu SAM WA UKWELI mpaka umauti ulipompata…

FULL STORY: Kifo cha Sam wa Ukweli aliomba afungwe Pampers

Soma na hizi

Tupia Comments