Video maarufu sana kwenye internet hivi sasa ni ya Jay Z akishambuliwa na shameji yake Solange ambayo tangu mtandao wa TMZ waipost May 12 imeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 9.
Taarifa mpya kuhusu hiyo video ni kwamba wauzaji waliinadi kutamfuta mteja atakayelipia pesa nyingi kununua video hiyo ambayo imekua gumzo.
Kati ya waliotaka kuinunua ni mtandao wa TMZ na ndio walioshinda kwa kulipa dola 250,000 (zaidi ya Tsh milioni 400) kupata video ya sekunde 58 isiyo na sauti na baadae video ya dakika 3 na sekunde 33 yenye sauti.
Mabosi wa hoteli hiyo walimpa kazi mwanasheria kuchunguza wakina nani waliitoa hiyo video yenye siri za wateja kwasababu ni watu wachache wanaruhusiwa kuingia kwenye chumba hicho ambapo hata hivyo taarifa za baadae zinasema alieitoa kafukuzwa kazi.
Unapenda chochote kinachonifikia kisikupite? jiunge na mimi twitter kwa kubonyeza HAPA pia facebook na Instagram kwa kubonyeza FB na INSTA ili nikutumie kila kitu, kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi.