Jay ameamua kuendelea kuonyesha ni jinsi gani amewekeza katika himaya ya burudani duniani baada ya jana kuingia mkataba na kampuni mpya inayojulika kwa jina la Tidal ambayo sasa atakuwa akinunua kazi za wasanii wengine na kuziuza kupitia kampuni hiyo.
Hivi karibuni Taylor Swift aliingia mkataba na Jay Z ambapo aliamua kuuza nyimbo zake zote.
Raper huyo katika uzinduzi huo uliofanyika New York aliamua kuwashirikisha wasanii wakubwa wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya muziki duniani ambao ndio waanzilishi katika kampuni hiyo.
Wasanii hao ni pamoja na Alicia Keys, Arcade Fire’s Win Butler na Régine Chassagne, Beyoncé, Daft Punk, Jack White, Jason Aldean, J. Cole, Kanye West, Deadmau5, Madonna, Nicki Minaj, Rihanna, Calvin Harris, Chris Martin na Usher.
Alicia Keys ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kwa ufupi kuwa lengo la kuungana ni kuhakikisha wanshirikiana kaika sauti moja na kuhakikisha wanaleta mapinduzi katika historia ya muziki kwa manufaa ya mashabiki na wasanii kwa ujumla.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook