Michezo

Unadhani kwa ushindi walioupata Real Madrid wanaweza kumwachia CHICHARITO aende?

on

ChicharitoReal Madrid imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuifunga bao 1-0 wapinzani wao Atletico Madrid kupitia kwa mshambuliaji Javier Hernandez ‘Chicharito’.

Ushujaa aliouonesha Chicharito huenda ukazaa matunda baada ya klabu ya Westham kutenga dau la euro milioni 7 ili iweze kunasa saini yake kwa ajili ya msimu ujao.

Ushindi wa Real Madrid umemweka Chicharito kwenye ramani nyingine na huenda akawaniwa na timu kubwa katika ligi kuu ya England.

Hata hivyo inaonekana ni vigumu Real Madrid kuruhusu kumwachia mshambuliaji huyo ambaye alipelekwa kwa mkopo Real Madrid akitokea Manchester United kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa na umuhimu wake ndani ya Klabu hiyo.

Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments