Tunayo stori kutokea kwa Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambapo amesema wilaya hiyo imedhamiria kujenga Shule ye kwanza ya Bweni ya Wasichana ikiwa ni mpango wa Kampeni ya Tokomeza Zero.
Akizungumza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) DC Jokate amesema shule hiyo itakuwa ya kidato cha kwanza hadi sita ikiwa ni ya kwanza kwa Kisarawe hasa kwa kuzingatia changamoto wanazokutana nazo watoto wakike.
“Mwaka huu tumejikita katika kujenga shule ya kwanza ya wasichana ambapo harambee yetu itafanyika Machi 30 mwaka huu Mlimani City ambapo tunatarajia uwepo wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,“amesema.