Top Stories

Jengo la utawala la Chuo cha Makerere lateketea kwa moto (+picha)

on

Taarifa kutoka Uganda  leo Septmber 20, 2020 ni moto mkubwa umezuka katika jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Makerere Jijini Kampala nchini Uganda usiku wa kuamkia leo.

Jengo hilo ni moja ya vivutio Jijini Kampala hivyo taarifa za kutokea kwa moto zimewaumiza wengi, hadi sasa chanzo na kiwango cha hasara iloyosababishwa na moto huo havijajulikana.

Ujenzi wa jengo hilo ulikamilika mwaka 1941 chini ya uongozi wa Mkuu wa Chuo, George C. Turner. Jengo hilo kuu ni moja ya kivutio kikubwa katika Jiji la Kampala, kutokana na muonekano wake kufanana na majengo ya Kiingereza.

Soma na hizi

Tupia Comments