Michezo

Ndondo Cup inatimiza ndoto ya Rabin Sanga, anaenda Besiktas Uturuki sasa

on

Rabin Sanaga ambaye ni kijana wa kitanzania aliyekuwa anacheza soka katika kituo cha kulelea wachezaji chipukizi cha Bom Bom SC, ndoto yake kama ilivyo ya wanasoka wengi kupata nafasi ya kucheza soka nje inaweza kutimia kutokana na anainza rasmi safari ya Ulaya weekend hii.

Baada ya kufanikiwa kuibuka mchezaji bora wa michuano ya Ndondo Academy 2018, Rabin kupitia wadhamini wa michuano ya Ndondo Cup ambao ni kampuni ya vifaa ya electorics Beko, walitangaza mchezaji bora atapelekwa kwenda kufanya majaribio katika club ya Besiktas ya nchini Uturuki.

Kwa maana hiyo basi Beko kwa kushirikiana na Clouds Media Group na Shadaka Sports Management, watatimiza ahadi hiyo weekend hii alfairi ya Jumapili ambapo Rabin Sanga akiambatana na mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda ataenda Uturuki katika club ya Besiktas kwa majaribio ya siku 10, Beko ndio wadhamini wakuu wa Besiktas.

Msimamo wa Beno Kakolanya Yanga ndio huu, katuma tena barua

Soma na hizi

Tupia Comments