Kada wa Chama Cha Mapinduzi Furaha Dominic leo July 21,2020 ameongoza kura za maoni Jimbo la Kawe Dar es salaam baada ya kupata kura 101 kati ya 474 zilizopigwa akifuatiwa na Angela Kiziga aliyepata kura 85.
Nafasi ya tatu imeshikwa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima aliyepata kura 79 huku aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, Kippi Warioba akipata kura tatu kati ya 475.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ameshika nafasi ya 4 kwa kupata kura 61, huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM mapema mwaka huu Vincent Mashinji amepata kura 2.