Serikali imepiga marufuku rasmi utengenezaji na uuzwaji wa Pombe ambazo hufungwa katika vifungashio vya mifuko ya plastiki maarufu kama “VIROBA” na kuagiza kuanzia sasa watengenzaji wa pombe hizo watafute utaratibu uliotengenezwa na serikali kwa kuzifunga katika chupa zinazoweza kurejeshwa.
Agizo hilo linasema zinatakiwa kuwa na ujazo usiopungua milligram 250 ambapo atakayebainika kukiuka masharti ya kanuni hizi atawajibishwa kulipa faini, kufungwa jela au yote kwa pamoja kwa mujibu wa kanuni.
Bonyeza play hapa chini kumtazama Waziri wa Muungano na Mazingira January Makamba akifafanua zaidi.
“Kuanzia March 1 Pombe za VIROBA Marufuku Tanzania” – Waziri Mkuu Majaliwa, Tazama full video hapa chini
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo