Duniani

Video ya mzee aliyesafiri kwa miezi saba pekeyake baharini kutoka Marekani..

on

Kwenye vitu ama stori ambazo zimeonekana kukamata vichwa vya habari vya kimataifa kwa saa kadhaa mfululizo pamoja na mitandao mikubwa, iko pia stori ya mzee mwenye umri wa miaka 53, jina lake ni John Beeden.

Mzee Joe alianza safari yake San Francisco Marekani siku ya June 1 2015 akiwa na boti yake ndogondogo na kufanikiwa kufika Jiji la Cairns Australia, siku ya jana December 27 2015… safari yake imekamilika kwa kusafiri jumla ya siku 209 ambazo kwa hesabu nyingine ni miezi saba kamili !!

Kwa umbali ambao mzee huyo amesafiri, hesabu zinaonesha kuwa amekuwa akisafiri kwa jumla ya saa 15 kila siku ambapo ina maana kwa siku alikuwa na saa kama tisa tu za kupumzika.

Stori yake iko pia kwenye hii video.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments