Tumezoea kumuona katika video mbalimbali akipewa shavu kimtindo, ‘Kings & Queens’ ya AY, baadae tukamsikia kwenye ‘Kaka na Dada’ aliyoshirikishwa na Lucci, jana ilikuwa birthday yake, naona kaona aitumie siku hiyo rasmi kutangaza anaingia kwenye muziki.
Hapo namzungumzia Jokate Mwegelo ana wimbo wake mpya ‘Leo Leo‘ ambao aliuachia jana katika show ya XXL.
Tunaona mastaa wa Bongo waliohit ndio wanafanya collabo na Wanigeria, Jokate kaanza na collabo Nigeria moja kwa moja- Feat Ice Prince.
Producer ni Mbongo wetu Tudd Thomas.
Tumia time yako kusikiliza collabo hiyo hapa mtu wangu…
Kama una chochote kuhusu wimbo huu unaweza kuacha hapa comment yako Kidoti atapitia hapa kuona mtu wake umemuandikia nini.