Mrembo Jokate Mwegelo aliteuliwa kuwa msemaji ramsi wa shindano la Miss Tanzania baada ya shindano hilo kupewa msamaha na BASATA baada ya kufungiwa toka mwishoni mwa mwaka 2014.
Kubwa ambalo amelisema alipohojiwa TZA kwenye studio za Millard Ayo ni maamuzi ya Miss Tanzania kufuta utaratibu wa mashindano ya kitongoji pamoja na mashindano ya kanda na sasa unarudishwa utaratibu wa zamani wa mashindano ya mikoa tu, yaani mfano Miss Arusha, Miss Tanga n.k alafu moja kwa moja kwenye ngazi ya taifa.
Jokate amesema mkoa wa Dar es Salaam pekee ndio utabaki na mashindano ya kanda kwenye sehemu tatu ambazo ni Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo shindano hili litaanza rasmi kuzisogelea headlines kubwa baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania kumalizika.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE