Jumamosi iliyopita ilikua harusi ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Lucas Muhavile maarufu kama Joti ambapo gumzo lilikua pia nywele zake alizonyoa kwa staili ya kiduku na kuingia nacho Kanisani jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuongea sana kwenye mitandao.
Leo AyoTV na millardayo.com zinae Joti kwenye Exclusive Interview ambapo amewajibu waliomsema kuhusu kiduku chake, >>> “Sidhani kama kuna sheria au kuna maandiko yameandika kwamba ukinyoa hivi hutakiwi kufunga ndoa, hii sanasana iko kwenye maadili tu“
“Nilimuomba Padri na akanielewa na kuniambia wewe ni Msanii tunajua cha kufanya usisuke tu, fumua hizo nywele ziwe tu kawaida zibanebane vizuri”
UNAWEZA KUMTAZAMA JOTI MWENYEWE KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: Harusi ya Joti na alivyoingia ukumbini kwa sebene… bonyeza play hapa chini kujionea
VIDEO: Orijino Komedi walivyoingia kwenye harusi ya Masanja wakiwa wamevaa sare za Polisi, bonyeza play hapa chini kutazama