Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kutoa ahadi ya shilingi milioni 5 za Kitanzania kwa ajili ya kuisadia familia ya Marehemu Godzilla hasahasa Mama mzazi wa Godzilla kwenye matibabu, sasa leo February 19,2019 ahadi hiyo imetimia.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Fid Q ameweka kipande cha video kikimuonyesha akikabidhi kitita cha pesa hizo taslimu kwa Mama mzazi wa marehemu nyumbani kwao Salasala na kusema kuwa amefanikiwa kufikisha pesa hizo salama.
“Alhamdullilah nilifanikiwa kuifikisha salama SALASALA kwa MAMA ile shilingi milioni TANO taslim toka kwa @baba_keagan – IN SHA ALLAH MWENYEZI atamuongezea pale palipopungua.. AMEN 🙏🏾 😇”
VIDEO: FLORA KAONGEA BAADA YA KUDAIWA KUMTOROSHA PASCAL WA BSS HOSPITALI