Wanandoa Beyonce na Jay Z wamesaidia kuongeza idadi ya watalii kwenye makumbusho ya Louvre jijini Paris nchini Ufaransa hadi kufikia jumla ya watalii Milioni 10.2 mwaka 2018 hii ni baada ya kufanya video ya ngoma yao “APES**T” ndani ya jengo hilo.
Inatajwa kuwa rekodi hiyo ni ya kipekee ikiwa imepita miaka sita eneo hilo halijawahi kupata idadi kubwa ya watalii hao ambapo mwaka 2012 jumla ya watalii waliotembelea makumbusho hiyo ni jumla ya watu Milioni 9.7 baada ya kufungua rasmi maonyesho ya michoro ya Leonardo da Vinci iliyochorwa mwaka 1503.
Mpaka sasa video ya ngoma hiyo imetazamwa na zaidi ya watu Milioni 147 kwenye mtandao wa YouTube tokea iachiwe rasmi June 16,2018.
MASTAA: Wema, Lulu, Masogange, Nandy na Billnass kwenye matukio 10 yaliyotikisa 2018