Alipoitoa audio ya single hii Jux aliulizwa kwenye XXL ya Clouds FM kama ni dedication kwa mpenzi wake aitwae Jackie Cliff anaedaiwa kufungwa jela nchini China kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya ambapo alijibu ‘yeah ina muhusu pia’
Siku kadhaa baadae pichaz zikaanza kuenea kwenye internet zikimuonyesha Jux akiwa China kuifanya video hiyo akiwa na msichana ambae kwenye hizo picha hakuonyeshwa sura kabisa na kwa sababu alikua ana umbo kama la Jackie, zilianza stori kwamba Jackie ataonekana kwenye video.
Hatimae kipisi kifupi cha hii video kimeachiwa wakati video kamili ikisubiriwa ambapo kwa kilichoonekana ndani yake sio Jackie Cliff ndio maana kila mtu anaisubiria video nzima.
Kipisi chenyewe kitazame hapa chini mtu wangu.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.