Michezo

Kaizer Chiefs wametangaza kocha mpya

on

Club ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini leo imemtambulisha Gavin Hunt ,56, raia wa Afrika Kusini kuwa ndiye kocha wao mkuu mpya.

Gavin amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Kaizer Chiefs, hiyo ikiwa zimepita siku chache toka timu hiyo imtimue alyekuwa kocha wao mkuu Ernst Middendorp raia wa Ujerumani pamoja na msaidizi wake Shaun Bartlett.

Kocha Gavin ambaye amewahi kuzichezea timu mbalimbali ikiwemo ya taifa ya Afrika Kusini, kabla ya kujiunga na Kaizer Chiefs alikuwa ni kocha wa Bidvest Wits kwa miaka 7 (2014-2020).

Soma na hizi

Tupia Comments