Jeshi la Polisi Nigeria limemsimamisha kazi mmoja wa Polisi wake maarufu na wanaoheshimika baada ya jina lake kujumuishwa kwenye Wanigeria wanaotuhumiwa kushirikiana na Mnigeria Ramon Abbas maarufu kama Hushpuppi ambae anakabiliwa na makosa ya utakatishaji alizokua akiiba kupitia mtandao.
Wanigeria mbalimbali walishtuka na taarifa za Polisi huyu Abba Kyari kuhusishwa na Hushpuppi kwani siku zote ameonekana ni Askari mwenye sifa nzuri na amekua akifanikisha mapambano mengi dhidi ya uhalifu.
Hadi sasa nyaraka za Mahakama Marekani zimeonesha kwamba Hushpuppi (37) ambae alikamatiwa Dubai, alisabishia Watu mbalimbali hasara ya USD milioni 24 (zaidi ya Tsh. Bilioni hamsini na tano).
Hata hivyo Kyari amesema hausiki na chochote kwenye madai hayo na kwamba mikono yake ni misafi, Ripoti zinasema kuwa kutokana na mashtaka dhidi yake… Hushpuppi anaweza kufungwa mpaka miaka 20 jela Nchini Marekani.
Hushpuppi aliekua akiishi Dubai na kutumia ukurasa wake wa Instagram wenye followers milioni 2.5 kuonesha maisha ya kifahari na magari ya bei mbaya, anatajwa na FBI kuwa ni mmoja wa watakatishaji fedha wakubwa wa dunia.
EXCLUSIVE: UKWELI KUHUSU DARAJA LA MITI LA MILIONI 31 MOROGORO