Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Magufuli ameweka wazi sababu iliyomfanya aliekuwa Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge kutopitishwa kugombea Ubunge kwa mara nyingine katika Jimbo hilo.
“Mzee Chenge hapa mimi ni Kaka yangu, wala sio uongo, nilipoingia Ubunge kwa mara ya kwanza Mwaka 1995 Mke wangu alikuwa na mimba, aliyenisaidia hela kwenda Hospitali Tsh Laki 2 alikuwa Mzee Chenge, ila kwa sasa zamu ya Ubunge ni ya mwingine maneno ya upinzani achaneni nayo” JPM
Nae Chenge akizungumza mbele ya JPM amesema “Nikushukuru JPM kwa heshima uliyonipa mbele ya Wananchi wa Bariadi, sikutegemea historia hiyo ya Mwaka 1995 ya mimi kukupa Tsh. Laki 2 wakati Mkeo akiwa Mjamzito ungeisema hapa mbele ya Watu wote, ila nakuhakikishia nitapambana kuwatafutia kura Wagombea wote”.