Top Stories

Kauli ya Serikali nyumbani kwa Mtoto aliefiwa na Familia yake yote ajalini (+video)

on

Serikali imesema itahakikisha Mtoto Anna Zambi anatimiza ndoto zake na anajengwa vizuri kisaikolojia baada ya kuondokewa na Wazazi wake wote wawili na Wadogo zake watatu waliofariki Tanga wakiwa njiani kwenda kwenye graduation yake.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Njingu amefika nyumbani kwa Familia ya Zambi Goba DSM na kusema tayari Maafisa wa Ustawi wa Jamii wameanza kumsaidia Anna kisaikolojia.

“Hata kama Mama yake Mdogo anamchukua kwenda kuishi nae hatutomuacha na tumeambiwa hata shuleni ana uwezo mkubwa sana, kwahiyo tunaamini atakuja kuwa rasimali muhimu sana katika Nchi yetu hatutokubali rasilimali ipotee” Dkt. Njingu

LUGOLA ATOA MAAGIZO MAZITO “POLISI KAMATA WATUMBUKIZE KWENYE PIPA LA MAJI YA KUWASHWAWASHA”

Soma na hizi

Tupia Comments