Michezo

Kelvin John apiga hat-trick KRC Genk vs Antwerp

on

Kinda wa Tanzania Kelvin John jana amefunga hat-trick katika ushindi wa 4-1 wa KRC Genk dhidi ya Royal Antwerp katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa vijana wa umri chini ya miaka 21 (U-21).

Kelvin John alianza kuiswazishia goli timu yake dakika 22, ikiwa ni dakika 4 zimepita toka Royal Antwerp wapate goli la utangulizi kupitia kwa Malik dakika ya 18, Kelvin akafunga tena magoli mawili dakika ya 29 na 70 na baadae dakika ya 92 Geusens akafunga goli la mwisho kwa Genk.


Huu ni mchezo wa 11 wa KRC Genk U-21 wakiwa wameshinda michezo 10 na sare 1 wakiongoza Ligi kwakuwa na alama 31 wakifuatiwa na Anderlecht U-21 wenye point 31 ila Genk wanaongoza kwa tofauti ya magoli.

Soma na hizi

Tupia Comments