Premier Bet
TMDA Ad

Stori Kubwa

Ishu ya kuhamia Dijitali Kenya hali si shwari, ziko TV zilizosimama kurusha matangazo..

on

7453_v8xVkE1a_o-600x337Kampuni tatu kubwa za utangazaji zimesitisha kurusha  matangazo kwenye televisheni kwa muda wa siku tatu baada ya Serikali kudhibiti mitambo ya zamani ya kurusha matangazo kwa mfumo wa analojia huku Kampuni hizo zikiwahakikishia waandishi wa habari kuwa hawatawafukuza kazi.

Kampuni hizo za Standard Media, inayomiliki television kibinafsi ya KTN na National Media Group inayomiliki NTV na QTV pamoja na Royal Media Services inayomiliki Citizen TV zimekuwa katika malumbano na Serikali ya Kenya kuhusu uhamiaji wa kurusha matangazo kwa kutumia mfumo wa digitali kutoka analojia.

Hata hivyo wasimamizi wa vituo hivyo wametumia njia ya mitandao kurusha matangazo yao, huku halmashauri ya Mawasiliano nchini humo  imewataka waende mahakamani ili kufikia muafaka juu ya wala hilo.

150216150807_runinga_3_za_kenya_zasitisha_matangazo_yao_512x288_bbc_nocredit

Sikiliza taarifa yote hapa niliyoirekodi wakati ikirushwa na kituo cha K 24.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram,  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments